muro98
muro98 logo
muro98

Atomic Habits: Utangulizi wa kitabu | Uchambuzi wa vitabu

James Clear akiwa amebobea katika masuala ya tabia na namna ya kuzibadilisha tabia, ameweka hoja ya kuwa "ubora wa maisha yetu huchangiwa kwa kiasi kikubwa na ubora wa tabia zetu". Na hoja hii aliyoiweka katika utangulizi wa kitabu chake ameithibitisha katika sura zilizofuata kwa kutumia ushahidi wa sayansi, falsafa na saikolojia ya wabobezi mbalimbali waliotangulia kwenye suala hili la tabia.

Yusuf Muro · 18 Mei 2025
Atomic

Wote tunapitia changamoto katika maisha. Na ni changamoto hizi ambazo zinatupa mafunzo muhimu yanayobaki na sisi milele. Mabadiliko madogo madogo tunayoyaanza kuyafanya ambayo mwanzoni huonekana kutokuwa na umuhimu huja baada ya muda kuleta tija na matokeo chanya ambayo humshangaza hata mhusika mwenyewe.

Haya ndio mawazo ya James Clear, mwandishi wa kitabu cha Atomic Habits aliyoyafikisha kwa undani katika utangulizi wa kitabu chake. Kitabu hichi ambacho kwa sasa kimeweza kuuza zaidi ya nakala milioni 20 na kutafsiriwa na lugha zaidi ya 60!

James Clear akiwa amebobea katika masuala ya tabia na namna ya kuzibadilisha tabia, ameweka hoja ya kuwa "ubora wa maisha yetu huchangiwa kwa kiasi kikubwa na ubora wa tabia zetu". Na hoja hii aliyoiweka katika utangulizi wa kitabu chake ameithibitisha katika sura zilizofuata kwa kutumia ushahidi wa sayansi, falsafa na saikolojia ya wabobezi mbalimbali waliotangulia kwenye suala hili la tabia.

Neno Tabia (Habits) amelielezea kuwa ni utaratibu ambao hufanywa mara kwa mara. Na kwa mujibu wa James Clear, tabia hizi licha ya kuwa ndogo ndogo kama vile kujijengea tabia ya kulala mapema, ratiba ya kusoma au kufanya mazoezi mara kadhaa kwa wiki zinapokuwa endelevu huleta matokeo makubwa na chanya.

Ushuhuda wa kwanza wa yote haya aliyoyazungumza ameutoa mwanzoni kabisa katika kitabu chake akianza kwa kuelezea tukio lililomtokea akiwa mwaka wa pili shuleni.

Tukio lenyewe ni la ajali iliyomtokea akiwa katika mchezo wa "baseball" ambapo fimbo inayotumika kupigia mpira wa mchezo huo ilipomponyoka mwanafunzi mwenzake na kwenda kumpiga usoni ikisababisha majeraha kadhaa eneo la pua na macho na mivunjiko kadhaa katika fuvu lake. Ajali hiyo mbaya ilimpelekea kupoteza fahamu na kupelekwa haraka hospitalini ambapo humo aliwekwa katika mashine kadhaa zilizomsaidia kupumua na baadae hali yake hiyo ilimhitaji kufanyiwa upasuaji. Ilimchukua miezi kadhaa tangu tukio hilo lilipotokea hadi hali yake kukaa sawa.

Muda wote huo hakuweza kujihusisha na mchezo huo ambao ulikuwa ni moja ya ndoto zake na hata alipopona ilimchukua muda kurudi na kuanza kucheza tena.

Lakini miiaka 6 tangu tukio hilo lilipomtokea aliweza kuwa mchezaji bora wa mchezo huo katika chuo alichosoma cha Denison na miaka kadhaa baadae aliweza kufanikiwa katika biashara yake na mafanikio ya safari yake ya uandishi yaliyompelekea kuandika kitabu hiki maarufu duniani cha

Atomic Habits. Mafanikio haya yote ameweza kuyaunganisha na tabia ndogondogo alizozijiwekea baada ya kupona na kufanya ziwe endelevu na anaamini mafunzo ya kitabu hiki yanaweza pia kukusaidia kubadilisha tabia yako na kutimiza malengo yako!

Muroblog tutaendelea kuchapisha makala haya kila jumapili tukichambua kitabu hiki sura moja hadi nyingine. Kwa maoni usisite kututumia barua pepe kwenda yusuf@muro98.com.

Kitabu hiki cha Atomic Habits na vingine vinapatikana sasa katika tovuti yetu— ingia sasa uagize kitabu chako! muro98.com/store.

muro98